YouVersion Logo
Search Icon

Isaya 63

63
Mungu awaadhibu maadui za watu wake
1 #63:1-6 Taz Isa 34:5-17; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14, 35:1-15; Amo 1:11-12; Ni nani huyu ajaye kutoka Edomu,
anayefika kutoka Bosra na mavazi ya madoa mekundu?
Ni nani huyo aliyevaa mavazi ya fahari,
anatembea kwa nguvu zake kubwa?
Ni mimi Mwenyezi-Mungu
ninayetangaza ushindi wangu;
nami ni mwenye nguvu ya kuokoa.
2Lakini mbona nguo yako ni nyekundu,
nyekundu kama ya mtu anayekamua zabibu?
3 #63:3 Taz Ufu 14:20, 19:13,15 “Naam, nimekamua zabibu peke yangu,
wala hakuna mtu aliyekuja kunisaidia.
Nimeyakanyaga mataifa kwa hasira yangu,
niliyapondaponda kwa ghadhabu yangu.
Nguo zangu zimejaa madoa ya damu yao,
imeyachafua kabisa mavazi yangu.
4Niliamua kuwa siku ya kulipiza kisasi imefika;
wakati wa kuwakomboa watu wangu umefika.
5 #63:5 Taz Isa 59:16 Nilitazama na hapakuwa na wa kunisaidia;
nilishangaa hapakuwa na wa kuniunga mkono.
Lakini nilijipatia ushindi kwa mkono wangu,
ghadhabu yangu ilinihimiza.
6Kwa hasira yangu niliwaponda watu,
niliwalewesha kwa ghadhabu yangu;
damu yao niliimwaga chini ardhini.”
Wema wa Mungu kwa Israeli
7Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu;
nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa,
kwa sababu ya yote aliyotutendea,
wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake,
kadiri ya wingi wa fadhili zake.
8Maana alisema juu yao:
“Hakika, hawa ni watu wangu;
watoto wangu ambao hawatanidanganya.”
Basi yeye akawa Mwokozi wao.
9Katika taabu zao zote,
hakumtuma mjumbe#63:9 … hakumtuma mjumbe … au Malaika; Yeye aliwaokoa. Yeye Mwenyewe alitaabika walipotaabika, akamtuma malaika wake awaokoe. mwingine kuwasaidia,
ila yeye mwenyewe alikuja kuwaokoa.
kwa upendo na huruma yake aliwakomboa.
Aliwabeba na kuwachukua tangu zamani.
10Lakini wao walikuwa wakaidi,
wakaihuzunisha roho yake takatifu.
Basi, Mungu akageuka, akawa adui yao;
yeye mwenyewe akapigana nao.
11Ndipo walipokumbuka#63:11 walipokumbuka: Kiebrania: Alipozikumbuka. siku za zamani,
wakati wa Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu.
Wakauliza, “Yuko wapi sasa Mwenyezi-Mungu,
aliyewaokoa wachungaji wa kundi lake baharini?
Yuko wapi yule aliyeiweka roho yake takatifu kati yao,
12 #63:12 Taz Kut 14:21 ambaye kwa mkono wake wenye nguvu
alifanya maajabu kwa njia ya Mose,
akapasua bahari na kuwaongoza watu wake,
na kujipatia jina la milele?
13Aliwaongoza katikati ya vilindi vya bahari,
wakapita humo kama farasi bila kujikwaa.
14Kama ng'ombe wapelekwavyo malishoni bondeni,
ndivyo roho ya Mungu ilivyowapumzisha watu wake.
Ndivyo ee Mungu ulivyowaongoza watu wako,
nawe ukajipatia jina tukufu.”
Sala ya kuomba msaada
15Ututazame kutoka mbinguni ee Mungu, uone,
utuangalie kutoka makao yako matakatifu na matukufu.
Iko wapi bidii yako kwa ajili yetu na nguvu yako?
Usiache kutuonesha upendo wako.#63:15 Usiache … upendo wako: Tafsiri ya neno kwa neno: Upendo na huruma yako vimezuiwa visionekane kwetu.
16Maana wewe ndiwe Baba yetu;
Abrahamu, mzee wetu, hatujali,
naye Israeli hatutambui;
lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ni Baba yetu.
Wewe umeitwa tangu kale: “Mkombozi wetu.”
17Ee Mwenyezi-Mungu, mbona unatukosesha njia zako?
Mbona unatufanya kuwa wakaidi hata tusikuogope?
Rudi ee Mungu kwa ajili ya watumishi wako,
makabila ambayo daima yalikuwa mali yako.
18Kwa kitambo tu sisi watakatifu wako tulimiliki nchi,
lakini maadui zetu wakaja wakaharibu maskani yako.#63:18 aya 18 makala ya Kiebrania si dhahiri.
19Tumekuwa kama watu ambao hujawatawala kamwe,
kama watu ambao hawakujulikana kwa jina lako.

Currently Selected:

Isaya 63: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy