YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 51

51
Kuomba usamehe
1-2Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi inayoelekea wakati nabii Natani alipomufikia kwa kumwonya juu ya uzinzi alioufanya na Batiseba.
3Unihurumie, ee Mungu,
kadiri ya wema wako;
uyafute makosa yangu,
kadiri ya wingi wa rehema yako.
4Unisafishe kabisa kosa langu;
unitakase zambi yangu.
5Ninaitikia kabisa makosa yangu,
siku zote ninaona waziwazi zambi yangu.
6Nimekukosea wewe peke yako,
nimetenda mabaya mbele yako.
Hivi uamuzi wako ni wa haki,
hukumu yako haipotoki. #Ang. Rom 3.4
7Mimi ni mukosaji tangia kuzaliwa kwangu,
mwenye zambi tangia tumbo la mama yangu.
8Wewe unataka moyo wa ukweli;
hivyo unifundishe kuwa na moyo wa hekima.
9Unitakase kwa hisopo,#51.9 Hisopo: Hisopo ni jina la mumea mumoja wenye majani madogo laini ambao ulitumiwa katika ibada za kutakasa kwa kunyunyiza maji au damu. nikuwe safi,
unisafishe, nikuwe mweupe pee.
10Unijaze furaha na shangwe,
unifurahishe tena, mimi ambaye uliniponda.
11Ugeuke, usiangalie zambi zangu;
uyafute makosa yangu yote.
12Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
uweke ndani yangu roho mupya na inayoimarika.
13Usinitupe mbali nawe;
usiondoe roho yako takatifu ndani yangu.
14Unirudishie furaha ya wokovu wako,
uniimarishe kwa Roho wako mwema.
15Halafu nitawafundisha wakosaji njia zako,
nao wenye zambi watarudi kwako.
16Uniokoe kutoka kosa la kumwanga damu,
ee Mungu, Mungu mwokozi wangu,
nami nitaimba kwa sauti kwamba umeniokoa.
17Ee Bwana, uniwezeshe kusema,
midomo yangu itangaze sifa zako.
18Kweli wewe haupendezwi na sadaka.
Hautaki nikutolee sadaka za kuteketezwa.
19Sadaka ninayokutolea, ee Mungu, ni roho munyenyekevu.
Haukatai moyo munyenyekevu na wa kutubu.
20Ee Mungu, upendezwe na kuutendea mazuri Sayuni;
uzijenge tena upya kuta za Yerusalema.
21Halafu utapendezwa na sadaka za haki:
ndizo sadaka za kuteketezwa na za kuteketezwa nzima.
Ngombe dume watatolewa juu ya mazabahu yako.

Currently Selected:

Zaburi 51: SWC02

Highlight

Copy

Compare

Share

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in