Zaburi 36
36
Uovu wa mwanadamu
1Kwa mukubwa wa waimbaji. Zaburi ya Daudi, mutumishi wa Yawe.
2Zambi inaongea na mutu mwovu,
ndani kabisa ya moyo wake;
kuogopa Mungu si kitu kwake. #Ang. Rom 3.18
3Mwovu anajipendelea mwenyewe,
anafikiri uovu wake hautagunduliwa na kulaaniwa.
4Kila anachosema ni uovu na uongo;
ameacha kutumia hekima na kutenda mema.
5Anapolala anawaza kutenda maovu,
anajiweka katika njia isiyokuwa nzuri,
wala hachukii uovu.
Wema wa Mungu
6Wema wako, ee Yawe, unaenea hata mbinguni;
uaminifu wako unafika hata kwenye mawingu.
7Haki yako ni kama milima mikubwa,
hukumu zako ni kama vilindi vya bahari.
Wewe, ee Yawe, unawalinda wanadamu na nyama.
8Kweli wema wako ni bora!
Wanadamu wanakimbilia kwenye kivuli cha mabawa yako.
9Unawashibisha kwa utajiri wa nyumba yako;
unawakunywesha katika muto wa wema wako.
10Wewe ndiwe asili ya uzima;
kwa mwangaza wako tunaona mwangaza.
11Uendelee kuwatendea mema wale wanaokutambua;
uzidi kuokoa wenye moyo wenye kunyooka.
12Usikubali wenye majivuno wanishambulie,
wala watu waovu wanikimbize.
13Kumbe watenda maovu wameanguka;
wameangushwa chini, hawawezi kuinuka.
Currently Selected:
Zaburi 36: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.