Hesabu 36
36
Urizi wa wanawake walioolewa
1Viongozi wa jamaa katika ukoo wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase mwana wa Yosefu, wakakwenda kuzungumuza na Musa na viongozi wengine wa ukoo za Waisraeli. 2Wakasema: Yawe alikuamuru kuwagawanyia watu wa Israeli inchi kwa kura kuwa urizi wao; alikuamuru vilevile uwape wabinti za Selofehadi ndugu yetu urizi wa baba yao. #Ang. Hes 27.7 3Lakini wao wakiolewa na Waisraeli wa makabila mengine, urizi wao utatoka kwetu na kuwaendea watu wa kabila watakamoolewa; kwa hiyo urizi wetu sisi utapunguka. 4Katika sikukuu ya ukumbusho urizi wao utahesabiwa pamoja na ule wa kabila watakamoolewa na hivyo kabila letu halitapata urizi huo tena.
5Basi, Musa akawapa Waisraeli agizo lile kutoka kwa Yawe, akawaambia: Watu wa ukoo wa kabila la Yosefu#36.5 kabila la Yosefu: ni kusema ukoo wa Manase, Ang. Hes 36.12. wamesema ukweli. 6Na hivi ndivyo Yawe anavyoamuru juu ya wabinti za Selofehadi; wako huru kuolewa na mutu yeyote wanayemupenda, lakini waolewe katika kabila lao, 7kusudi urizi wa Waisraeli usihamishiwe kwa kabila lingine; kila Mwisraeli atabakia na urizi wa kabila lake. 8Mwanamuke yeyote mwenye urizi katika kabila moja la Israeli anapaswa kuolewa na mutu wa kabila lake, kusudi kila Mwisraeli abakie na urizi wa babu zake. 9Hivyo hakutakuwa urizi wowote utakaohamishwa kutoka kabila moja kwa lingine. Kila kabila la Waisraeli litashikilia urizi wake.
10Wabinti za Selofehadi wakafanya kama vile Yawe alivyomwamuru Musa. 11Wote: Mala, Tirsa, Hogla, Milka na Noa wakaolewa na binamu zao. 12Wakaolewa katika jamaa za ukoo wa Manase mwana wa Yosefu, na urizi wao ukabaki katika kabila la baba yao.
13Hizo ndizo amri na maagizo ambayo Yawe aliwapa Waisraeli kwa njia ya Musa katika mabonde ya Moabu, ngambo ya muto Yordani karibu na muji wa Yeriko.
Currently Selected:
Hesabu 36: SWC02
Highlight
Share
Compare
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.