Hesabu 26
26
Hesabu ya Pili
1Kisha ule ugonjwa, Yawe akamwambia Musa na Eleazari mwana wa kuhani Haruni. #Ang. Hes 1.1-46 2Muhesabu Waisraeli wote, kila mutu kufuatana na jamaa yake. Muwahesabu watu wote wenye umri wa miaka makumi mbili na zaidi wanaofaa kwenda katika jeshi. 3Musa na kuhani Eleazari wakazungumuza na watu kwenye inchi za mabonde za Moabu, ngambo ya muto Yordani, karibu na Yeriko, wakawaambia: 4Muhesabu watu kuanzia na wenye umri wa miaka makumi mbili na zaidi, kama vile Yawe alivyomwamuru Musa. Hesabu ya Waisraeli waliotoka Misri ni hii:
5Kwanza ni kabila la Rubeni, muzaliwa wa kwanza wa Yakobo. Hanoki, Palu, 6Hesironi na Karmi. 7Hizo ndizo ukoo za kabila la Rubeni. Hesabu ya wanaume waliohesabiwa ni elfu makumi ine na tatu, mia saba na makumi tatu. 8Wazao wa Palu walikuwa Eliabu, 9na wana wake Nemueli, Datani na Abiramu. Hawa wawili: Datani na Abiramu, ndio waliokuwa wamechaguliwa, lakini wakamupinga Musa na Haruni, na kujiunga na wafuasi wa Kora wakati walipomwasi Yawe. 10Wakati huo udongo ukafunguka ikawameza, wakakufa pamoja na Kora na wafuasi wake moto ulipoangamiza watu mia mbili makumi tano; wakakuwa onyo kwa watu. 11Pamoja na hayo wana wa Kora hawakukufa.
12Kabila la Simeoni. Nemueli, Yamini, Yakini, 13Zera na Sauli. 14Hizo ndizo ukoo za kabila la Simeoni, jumla yao wanaume elfu makumi mbili na mbili mia mbili.
15Kabila la Gadi lilikuwa na jamaa za Sefoni, Hagi, Suni, 16Ozini, Eri, 17Arodi na Areli. 18Hizo ndizo ukoo za kabila la Gadi, jumla wanaume elfu makumi ine mia tano.
19Kabila la Yuda lilikuwa na Eri na Onani. Hawa walikufia katika inchi ya Kanana. 20Kabila la Yuda lilikuwa na jamaa za Sela, Peresi, na Zera. 21Kutoka kwa Peresi, jamaa ya Hesironi na Hamuli. 22Hizo ndizo ukoo za Yuda, jumla wanaume elfu makumi saba na sita mia tano.
23Kabila la Isakari lilikuwa na jamaa za Tola, Puva, 24Yasubu na wa Simironi. 25Hizo ndizo ukoo za Isakari, jumla wanaume elfu makumi sita na ine mia tatu.
26Kabila la Zebuluni lilikuwa na jamaa za Seredi, wa Eloni na wa Yaleli. 27Hizo ndizo ukoo za Zebuluni, jumla wanaume elfu makumi sita mia tano.
28Kabila la Yosefu baba ya Manase na Efuraimu.
29Kabila la Manase lilikuwa na jamaa ya: Makiri, Gileadi, 30Yezeri, Heleki, 31Asirieli, Sekemu, 32Semida na Heferi. 33Selofehadi mwana wa Heferi hakupata watoto wanaume lakini wanawake tu, nao ni Mala, Noa, Hogula, Milka na Tirsa. 34Hizo ndizo ukoo za Manase, jumla wanaume elfu makumi tano na mbili mia saba.
35Kabila la Efuraimu lilikuwa na jamaa za Sutela, Bekeri na Tahani. 36Ukoo wa Erani ulikuwa na jamaa ya Sutela. 37Hizo ndizo ukoo za Efuraimu, jumla wanaume elfu makumi tatu na mbili mia tano. Zote hizo zilitokana na Yosefu.
38Kabila la Benjamina lilikuwa na jamaa za Bela, Asibeli, Ahiramu, 39Sufamu na Hufamu. 40Ukoo za Ardi na Namani, zilitokana na Bela. 41Hizo ndizo ukoo za Benjamina, jumla wanaume elfu makumi ine na tano mia sita.
42Kabila la Dani lilikuwa na jamaa ya Suhamu; 43ukoo ulikuwa na wanaume elfu makumi sita na ine mia ine.
44Kabila la Aseri lilikuwa na jamaa za Imuna, Isiwi na Beria. 45Ukoo za Heberi na Malkieli zilitokana na Beria. 46Aseri alikuwa na binti aliyeitwa Sera. 47Hizo ndizo ukoo za kabila la Aseri, jumla wanaume elfu makumi tano na tatu mia ine.
48Kabila la Nafutali lilikuwa na jamaa za Yaseli, Guni, 49Yeseri na Silemu. 50Hizi ndizo ukoo za kabila la Nafutali, jumla wanaume elfu makumi ine na tano mia ine.
51Hesabu ya wanaume Waisraeli waliohesabiwa ilikuwa elfu mia sita, na moja mia saba na makumi tatu.
52Kisha Yawe akamwambia Musa: #Ang. Hes 34.13; Yos 14.1-2 53Makabila haya yatagawanyiwa inchi ikuwe urizi wao, kulingana na hesabu ya majina yao. 54Kabila kubwa litapewa sehemu yao kubwa na dogo litapewa sehemu yao ndogo. Kila kabila litapewa urizi wake kulingana na hesabu ya watu wake. 55Hata hivyo ugawanyaji wa inchi utafanywa kwa kura. Kila kabila litarizi kulingana na majina ya ukoo wao. 56Urizi wa kila kabila utagawanywa kwa kura, kila kabila litapata kulingana na ukubwa au udogo wake.
57Hizi ndizo ukoo za Walawi zilizohesabiwa na jamaa zao Gersoni, Kohati na Merari, 58pamoja na jamaa za Libini, Hebroni, Mali, Musi na Kora. Kohati alikuwa baba ya Amuramu. 59Muke wa Amuramu aliitwa Yokebedi binti ya Lawi, aliyezaliwa Misri. Huyu alimuzalia Amuramu watoto wawili wanaume, Haruni na Musa, na binti mumoja, Miriamu. 60Haruni alikuwa na watoto wanaume wane, Nadabu, Abihu, Eleazari na Itamari. #Ang. Hes 3.2 61Nadabu na Abihu walikufa walipomutolea Yawe sadaka ya moto usiofaa. #Ang. Law 10.1-2; Hes 3.4 62Hesabu ya Walawi wanaume wenye umri wa mwezi mumoja na zaidi ilikuwa elfu makumi mbili na tatu. Hawa hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu wao hawakupewa urizi wowote kati yao.
63Hao ndio wanaume Waisraeli waliohesabiwa na Musa na kuhani Eleazari katika inchi za mabonde za Moabu, ngambo ya muto Yordani, karibu na Yeriko. 64Kati yao hakukuwa hata mutu mumoja aliyebakia kati ya wale waliohesabiwa na Musa na kuhani Haruni ambao walifanya hesabu ya kwanza katika jangwa la Sinai. 65Yawe alikuwa amesema kwamba wote watakufia katika jangwa, na kweli hakuna hata mumoja wao aliyebaki muzima, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. #Ang. Hes 14.26-35
Currently Selected:
Hesabu 26: SWC02
Highlight
Share
Compare
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.