YouVersion Logo
Search Icon

Yoeli UTANGULIZI

UTANGULIZI
Hatujui mengi juu ya mambo yanoyoelekea huyu nabii Yoeli zaidi ya yale tunayoambiwa kwa ufupi sana kwa mwanzo wa kitabu hiki, wala hatuwezi kusema kwa uhakika aliishi nyakati gani.
Mwanzo wa kitabu hiki kinaonyesha namna inchi ilivyoharibiwa na nzige pamoja na kukauka kwa maji. Yoeli anaona na kutangaza kwamba ni kitambulisho cha kuja kwa Siku ya Yawe. Kwake ni wazi kwamba Mungu atakamata mupango wa kuwaazibu wote wanaopinga mapenzi yake.
Yoeli anataka watu warudilie Mungu kikamilifu. Anasema juu ya wakati Mungu atakapowashushia watu wote Roho wake, wanaume na wanawake, watoto na wazee (3.1-5). Katika Agano Jipya ahadi hiyo ya Mungu imepangwa kukamilika kwa kuja kwa Roho Mutakatifu (angalia Matendo 2.17-21).

Currently Selected:

Yoeli UTANGULIZI: SWC02

Highlight

Share

Compare

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in