Yobu 26
26
Jibu la Yobu
1Kisha Yobu akajibu:
2Aa! Jinsi gani ulivyomusaidia asiyekuwa na uwezo!
Jinsi gani ulivyomwokoa asiyekuwa na nguvu!
3Jinsi gani ulivyomushauri asiyekuwa na hekima,
na kumushirikisha ujuzi wako!
4Lakini umesema hayo kwa ajili ya nani?
Nani aliyekusukuma kuongea hivyo?
Bildadi anasema
5Mizimu kule chini inatetemeka,
maji ya chini na wakaaji wake yanaogopa.
6Kuzimu kuko wazi kabisa mbele ya Mungu.
Shimo la kuangamia halina kifuniko chochote.
7Mungu anatandaza kaskazini juu ya pahali patupu,
na anatundika dunia pahali pasipo kuwa kitu.
8Anayafunga maji katika mawingu yakuwe mazito,
nayo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
9Anaufunika uso wa mwezi
na kutandaza juu yake wingu.
10Amechora muviringo juu ya uso wa bahari,
penye mpaka kati ya mwangaza na giza.
11Mungu akitoa sauti ya kukaripa,
nguzo za mbingu zinatetemeka na kushangaa.
12Kwa nguvu zake alituliza bahari;
kwa maarifa yake alimwangamiza Rahabu.
13Kwa pumzi yake alisafisha anga;
mukono wake ulitoboa nyoka mukubwa anayeruka.
14Ikiwa haya ni machache tu ya matendo yake,
ni minongono tu tunayosikia juu yake,
nani anayeweza kujua ukubwa wa nguvu yake?
Yobu anaendelea kusema
Currently Selected:
Yobu 26: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.