YouVersion Logo
Search Icon

Kutoka 20

20
Amri kumi
(Kumb 5.1-21)
1Mungu alisema maneno haya yote:
2Mimi ni Yawe, Mungu wako, niliyekutoa katika inchi ya Misri, ambako ulikuwa mutumwa.
3Usikuwe na miungu mingine isipokuwa mimi.#20.3 au: Usikuwe na miungu mingine zaidi yangu.
4Usijifanyie sanamu ya miungu, wala mufano wa kitu chochote kinachokuwa juu mbinguni, wala kinachokuwa chini katika dunia, wala kinachokuwa ndani ya maji chini ya dunia. #Ang. Kut 34.17; Law 19.4; 26.1; Kumb 4.15-18; 27.15 5Usiiname mbele yao wala kuvitumikia, kwa sababu mimi Yawe, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Ninawaazibu wana kwa ajili ya maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha ine cha wale wanaonichukia. #Ang. Kut 34.6-7; Hes 14.18; Kumb 7.9-10 6Lakini ninawatendea mema maelfu ya wale wanaonipenda na kushika amri zangu.
7Usitaje bure jina langu mimi Yawe, Mungu wako, maana mimi Yawe sitaacha kumwazibu yeyote anayetaja bure jina langu. #Ang. Law 19.12
8Usisahau kuiweka takatifu siku ya Sabato. #Ang. Kut 16.23-30; 31.12-14 9Siku sita fanya kazi na tenda mambo yako yote. 10Lakini siku ya saba ni Sabato ya Yawe, Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mutumwa wako, wala mujakazi wako, wala nyama wako wa kufugwa, wala mugeni anayekuwa katika nyumba yako. 11Maana kwa siku sita mimi Yawe niliumba mbingu na inchi, bahari na vyote vinavyokuwa ndani yake, kisha nikapumzika siku ya saba. Kwa hiyo mimi Yawe nilibariki siku ya Sabato, nikaitakasa.
12Uwaheshimu baba yako na mama yako, kusudi uishi maisha marefu katika inchi ninayokupatia mimi Yawe, Mungu wako. #Ang. Kumb 27.16; Mat 15.4; 19.19; Mk 7.10; 10.19; Lk 18.20; Efe 6.2-3
13Usiue. #Ang. Mwa 9.6; Law 24.17; Mat 5.21; 19.18; Mk 10.19; Lk 18.20; Rom 13.9; Yak 2.11
14Usizini. #Ang. Law 20.10; Mat 5.27; 19.18; Mk 10.19; Lk 18.20; Rom 13.9; Yak 2.11
15Usiibe. #Ang. Law 19.11; Mat 19.18; Mk 10.19; Lk 18.20; Rom 13.9
16Usimushuhudie mwenzako uongo. #Ang. Kut 23.1; Mat 19.18; Mk 10.19; Lk 18.20
17Usitamani nyumba ya mwenzako, wala muke wake, wala mutumwa wake au mujakazi wake, wala ngombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote mwenzako anachokuwa nacho. #Ang. Rom 7.7; 13.9
18Watu waliposikia ngurumo na kuona umeme ukiwaka na kusikia sauti ya baragumu juu ya mulima uliokuwa unafuka moshi, wote wakaogopa na kutetemeka. Wote wakasimama mbali, #Ang. Ebr 12.18-19 19wakamwambia Musa: Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini Yawe asiseme nasi, tusikufe.
20Musa akawaambia: Musiogope, maana Mungu amekuja kuwapima kusudi mupate kumwogopa siku zote na musitende zambi.
21Watu wote wakasimama mbali wakati Musa alipokaribia lile wingu zito Mungu alimokuwa.
22Yawe akamwambia Musa: Uwaambie Waisraeli: Mumejionea ninyi wenyewe kwamba nimeongea nanyi kutoka mbinguni. 23Mutaniheshimu mimi peke yangu wala musijifanyie miungu ya feza wala ya zahabu. 24Ninyi mutanijengea mazabahu ya udongo. Juu yake mutanitolea kondoo wenu na ngombe wenu kama sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani. Pahali popote nitakapowakumbusha watu jina langu, pale pale mimi mwenyewe nitawafikia na kuwabariki. 25Kama mukinijengea mazabahu ya mawe, musiitengeneze kwa mawe ya kuchonga, maana mukitumia vyombo vya kuchonga mawe, mutaichafua. #Ang. Kumb 27.5-7; Yos 8.31 26Wala musitengeneze mazabahu yenye ngazi za kupandia, mutu asipate kuona uchi wa yule anayepanda juu yake.

Currently Selected:

Kutoka 20: SWC02

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in