YouVersion Logo
Search Icon

Zab 8

8
Utukufu wa Mungu na Hadhi ya Utu
Kwa mwimbishaji: kwa kufuata Gitithi. Zaburi ya Daudi.
1Wewe, MUNGU, Bwana wetu
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
2 # Mt 21:16; 11:25; 1 Kor 1:27 Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao
Umeiweka misingi ya nguvu;
Kwa sababu yao wanaoshindana nawe;
Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi.
3 # Zab 44:16; 19:1; Ayu 22:12; Rum 1:20 Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako,
Mwezi na nyota ulizoziratibisha;
4 # Ayu 7:17-18; Zab 144:3; Ebr 2:6-8 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke,
Na binadamu hata umwangalie?
5Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu;
Umemvika taji ya utukufu na heshima;
6 # 1 Kor 15:27; Efe 1:22; Ebr 2:8; Mwa 1:26 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
7Kondoo, na ng’ombe wote pia;
Naam, na wanyama wa kondeni;
8Ndege wa angani, na samaki wa baharini;
Na kila kipitacho njia za baharini.
9 # Ayu 11:7; Zab 35:10 Wewe, MUNGU, Bwana wetu,
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!

Currently Selected:

Zab 8: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy