YouVersion Logo
Search Icon

Zab 7

7
Ombi la Msaada dhidi ya Watesaji
Ombolezo la Daudi, aliloimba kwa BWANA kuhusu Kushi, Mbenyamini.
1BWANA, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe,
Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye.
2 # 1 Pet 5:8 Asije akaipapura nafsi yangu kama simba,
Akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya.
3 # 2 Sam 16:7 BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya,
Ikiwa mna uovu mikononi mwangu,
4 # 1 Sam 24:7 Ikiwa nimemlipa mabaya
Yeye aliyekaa kwangu salama;
(Hasha! Nimemponya yeye
Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;)
5Basi adui na anifuatie,
Na kuikamata nafsi yangu;
Naam, aukanyage uzima wangu,
Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.
6 # Zab 94:2 BWANA uondoke kwa hasira yako;
Ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu;
Uamke kwa ajili yangu;
Umeamuru hukumu.
7Kusanyiko la mataifa na likuzunguke,
Na juu yake uketi utawale.
8BWANA atawaamua mataifa,
BWANA, unihukumu mimi,
Kwa kadiri ya haki yangu,
Sawasawa na unyofu nilio nao.
9 # Ufu 2:23; 1 Sam 16:7 Ubaya wao wasio haki na ukome,
Lakini umthibitishe mwenye haki.
Kwa maana mjaribu mioyo na viuno
Ndiye Mungu aliye mwenye haki.
10Ngao yangu ina Mungu,
Awaokoaye wanyofu wa moyo.
11Mungu ni mwamuzi mwenye haki,
Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku.
12Mtu asiporejea ataunoa upanga wake;
Ameupinda uta wake na kuuweka tayari;
13Naye amemtengenezea silaha za kufisha,
Akifanya mishale yake kuwa ya moto.
14Tazama, huyu ana utungu wa uovu,
Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.
15 # Est 7:10; Mit 5:22 Amechimba shimo, amelichimba chini sana,
Akatumbukia katika handaki aliyoifanya!
16 # 1 Fal 2:32 Madhara yake yatamrejea kichwani pake,
Na dhuluma yake itamshukia utosini.
17Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake;
Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu.

Currently Selected:

Zab 7: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy