YouVersion Logo
Search Icon

Lk 1:57, 58, 59, 60, 61, 62, 63, 64, 65, 66, 67, 68, 69, 70, 71, 72, 73, 74, 75, 76, 77, 78, 79, 80

Lk 1:57 SUV

Ikawa, siku za kuzaa kwake Elisabeti zilipotimia, alizaa mtoto mwanamume.

Lk 1:59 SUV

Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria.

Lk 1:60 SUV

Mamaye akajibu akasema La, sivyo; bali, ataitwa Yohana.

Lk 1:61 SUV

Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa zako aitwaye jina hilo.

Lk 1:62 SUV

Wakamwashiria babaye wajue atakavyo kumwita.

Lk 1:63 SUV

Akataka kibao, akaandika ya kwamba, Jina lake ni Yohana. Wakastaajabu wote.

Lk 1:64 SUV

Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake pia, akaanza kunena akimsifu Mungu.

Lk 1:67 SUV

Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema

Lk 1:68 SUV

Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.

Lk 1:69 SUV

Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.

Lk 1:70 SUV

Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu

Lk 1:71 SUV

Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia

Lk 1:72 SUV

Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu

Lk 1:73 SUV

Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu

Lk 1:74 SUV

Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu

Lk 1:75 SUV

Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zetu zote.

Lk 1:77 SUV

Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao.

Lk 1:78 SUV

Kwa njia ya rehema za Mungu wetu, Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia

Lk 1:79 SUV

Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy