YouVersion Logo
Search Icon

Kum 33

33
Baraka ya Mwisho ya Musa kwa Israeli
1 # Mwa 49:28; Lk 24:50; Yn 14:27; 16:33 Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake. 2#Kut 19:18; Amu 5:4; Hab 3:3; Dan 7:10; Mdo 7:53; Gal 3:19; Ebr 2:2Akasema,
BWANA alitoka Sinai,
Akawaondokea kutoka Seiri;
Aliangaza katika kilima cha Parani,
Akaja Meribath-kadeshi.
Upande wa mkono wake wa kuume
Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.
3 # Hos 11:1; Mal 1:2; 1 Sam 2:9; Zab 50:5; Lk 10:39; Mdo 22:3 Hakika awapenda hayo makabila ya watu;
Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako;
Nao waliketi miguuni pako;
Watapokea kila mmoja katika maneno yako.
4 # Yn 7:19 Musa alituagiza torati,
Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo.
5 # Ayu 29:25 Akawa mfalme katika Yeshuruni,
Walipokutanika wakuu wa watu,
Makabila yote ya Israeli pamoja.
6Reubeni na aishi, asife;
Lakini watu wake na wawe wachache.
7 # Mwa 49:8 Na baraka ya Yuda ni hii; akasema,
Isikize, Ee BWANA, sauti ya Yuda,
Umlete ndani kwa watu wake;
Alijitetea kwa mikono yake;
Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake.
8 # Kut 17:7; 28:30; Hes 20:13; 27:21; Law 8:8 Akamnena Lawi,
Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako,
Uliyemjaribu huko Masa;
Ukateta naye kwenye maji ya Meriba.
9 # Kum 13:6; Mt 10:37; 12:48; Mk 10:29; Lk 14:26; Kut 32:26; Yer 18:18; Mal 2:5 Aliyemtaja baba yake na mama yake, Mimi sikumwona;
Wala nduguze hakuwakubali;
Wala hakuwajua watoto wake mwenyewe;
Maana wameliangalia neno lako,
Wamelishika agano lako.
10 # Law 10:11; Kut 30:7,8; Zab 51:19 Watamfundisha Yakobo hukumu zako,
Na Israeli torati yako,
Wataweka uvumba mbele zako,
Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako.
11 # Zab 20:3 Ee BWANA, ubariki mali zake,
Utakabali kazi ya mikono yake;
Uwapige viuno vyao waondokao juu yake,
Na wenye kumchukia, wasiinuke tena.
12Akamnena Benyamini,
Mpenzi wa BWANA atakaa salama kwake;
Yuamfunika mchana kutwa,
Naye hukaa kati ya mabega yake.
13 # Mwa 49:25; 27:28 Na Yusufu akamnena,
Nchi yake na ibarikiwe na BWANA;
Kwa vitu vya thamani vya mbinguni, kwa huo umande,
Na kwa kilindi kilalacho chini,
14Na kwa vitu vilivyo bora vya matunda ya jua,
Na kwa vitu vilivyo bora vya maongeo ya miezi,
15 # Hab 3:6 Na kwa vitu viteule vya milima ya kale,
Na kwa vitu vilivyo bora vya vilima vya milele,
16 # Kut 3:2,4; Mdo 7:30 Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake,
Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kijiti;
Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu,
Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze.
17 # 1 Fal 22:11; Zab 44:5 Mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe wake mume, enzi ni yake;
Na pembe zake ni pembe za nyati;
Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi;
Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu,
Nao ni maelfu ya Manase.
18Na Zabuloni akamnena,
Furahi Zabuloni, katika kutoka kwako;
Na Isakari, katika hema zako.
19 # Isa 2:3; Yer 50:4,5; Zab 4:5 Watayaita mataifa waje mlimani;
Wakasongeze huko sadaka za haki;
Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari,
Na akiba zilizofichamana za mchangani.
20 # Yos 13:10; 1 Nya 12:8 Na Gadi akamnena,
Na abarikiwe amwongezaye Gadi;
Yeye hukaa kama simba mke,
Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.
21 # Hes 32:16,21; Yos 4:12 Akajichagulia sehemu ya kwanza,
Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria;
Akaja pamoja na wakuu wa watu,
Akaitekeleza haki ya BWANA,
Na hukumu zake kwa Israeli.
22 # Yos 19:47; Amu 18:27 Na Dani akamnena,
Dani ni mwana-simba,
Arukaye kutoka Bashani.
23 # Yos 19:32 Na Naftali akamnena,
Ee Naftali, uliyeshiba fadhili,
Uliyejawa na baraka ya BWANA;
Umiliki magharibi na kusini.
24 # Ayu 29:6 Na Asheri akamnena,
Na abarikiwe Asheri kwa watoto;
Na akubaliwe katika nduguze,
Na achovye mguu wake katika mafuta.
25Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba;
Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.
26 # Kut 15:11; Zab 86:8; Yer 10:6; Zab 68:4,33,34; 104:3; Hab 3:8 Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni,
Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie.
Na juu ya mawingu katika utukufu wake.
27 # Zab 90:1 Mungu wa milele ndiye makazi yako,
Na mikono ya milele i chini yako.
Na mbele yako amemsukumia mbali adui;
Akasema, Angamiza.
28 # Hes 23:9; Yer 23:6; 33:16 Na Israeli anakaa salama,
Chemchemi ya Yakobo peke yake,
Katika nchi ya ngano na divai;
Naam, mbingu zake zadondoza umande.
29 # Zab 144:15; 2 Sam 7:23 U heri, Israeli.
Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA!
Ndiye ngao ya msaada wako,
Na upanga wa utukufu wako;
Na adui zako watajitiisha chini yako,
Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.

Currently Selected:

Kum 33: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy