YouVersion Logo
Search Icon

2 Tim 4

4
1 # Mdo 10:42; 1 Pet 4:5; Rum 14:9,10 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; 2#Mdo 20:20,31lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 3#2 Tim 1:13; 1 Tim 4:1Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; 4#1 Tim 4:7; 2 The 2:11nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. 5#2 Tim 2:3; Efe 4:11Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. 6#Flp 2:17Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. 7#1 Kor 9:25; 1 Tim 6:12; Flp 3:14Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8#2 Tim 2:5; Yn 1:22; 1 Pet 5:4; Ufu 2:10baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
Maagizo ya Kibinafsi
9 # 2 Tim 1:4 Jitahidi kuja kwangu upesi. 10#2 Kor 8:23; Gal 2:3; Kol 4:14; Tit 1:4; Flm 1:24Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia. 11#Mdo 12:12,25; 13:13; 15:37-39; Kol 4:10,14; Flm 1:24Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi. 12#Mdo 20:4; Efe 6:21-22; Kol 4:7-8Lakini Tikiko nalimpeleka Efeso. 13#Mdo 20:6Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi. 14#Zab 28:4; 62:12; Mit 24:12; Rum 2:6; 1 Tim 1:20; 2 Sam 3:39Iskanda, mfua shaba, alionyesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake. 15Nawe ujihadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu. 16#2 Tim 1:15Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17#Zab 22:21; Dan 6:21,28; Mdo 23:11; 27:23Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. 18Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.
Salamu za Mwisho na Baraka
19 # Mdo 18:2; 2 Tim 1:16-17 Nisalimie Priska na Akila, na wale wa nyumbani mwa Onesiforo. 20#Mdo 19:22; 20:4; 21:29; Rum 16:23Erasto alikaa Korintho. Trofimo nalimwacha huko Mileto, hawezi. 21Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi. Eubulo akusalimu, na Pude, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia.
22Bwana na awe pamoja na roho yako. Neema na iwe pamoja nanyi.

Currently Selected:

2 Tim 4: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy