YouVersion Logo
Search Icon

2 Tim 3

3
Uovu katika Siku za Mwisho
1 # 1 Tim 4:1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. 2#Rum 1:29Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, 3wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, 4#Flp 3:19wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; 5#Mt 7:15,21; Rum 2:20; Tit 1:16wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. 6#Mt 23:14; Tit 1:11Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; 7#2 Tim 2:25wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli. 8#Kut 7:11,22; 1 Tim 6:5; 1:12Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani. 9Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
Mausia ya Paulo kwa Timotheo
10Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu, 11#Mdo 13:14-52; 14:1-20; Zab 34:19na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote. 12#Mt 16:24; Mdo 14:22Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. 13#1 Tim 4:1lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 14#2 Tim 2:2Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; 15#Yn 5:39; Zab 119:99na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. 16#2 Pet 1:19-21; Rum 15:4Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 17#1 Tim 6:11ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

Currently Selected:

2 Tim 3: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy