2 Wathesalonike Utangulizi
Utangulizi
Waraka huu uliandikwa miezi michache tu baada ya ule wa kwanza. Baadhi ya watu walikuwa wamemwelewa vibaya Paulo, au waraka mwingine wa bandia uliosemekana kuwa ulitoka kwa Paulo ulikuwa umewafadhaisha Wathesalonike kuhusu kurudi kwa Yesu. Paulo aliandika waraka huu ili kuwakumbusha yale aliyokuwa ametangulia kuwafundisha, akiwahakikishia waumini kuwa Kristo atarudi kuwafariji waliomwamini na kuwaadhibu wale waliokuwa wakiwatesa. Aliwaambia kwamba siku ya Bwana, yaani siku ya hukumu, haingewafikia mara moja, bali ingetanguliwa na matukio mbalimbali. Wakifahamu kuwa hakika Kristo angerudi, iliwapasa waumini kuishi maisha matakatifu yasiyo na lawama.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kuondoa mkanganyiko kuhusu kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili.
Mahali
Korintho.
Tarehe
Mnamo 51–52 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Silvano na Timotheo.
Wazo Kuu
Kuwafariji Wathesalonike kwa ajili ya mateso, na kuwahimiza waishi maisha ya kumtukuza Mungu.
Mambo Muhimu
Kurudi kwa Yesu Kristo, na kuwaonya waumini wasiache kufanya kazi.
Yaliyomo
Faraja kutokana na kurudi kwa Kristo (1:1‑12)
Matukio kabla ya kuja kwa siku ya Bwana (2:1–3:5)
Mausia ya Kikristo, na kuwatakia heri (3:6‑18).
ที่ได้เลือกล่าสุด:
2 Wathesalonike Utangulizi: NEN
เน้นข้อความ
คัดลอก
เปรียบเทียบ
แบ่งปัน
ต้องการเน้นข้อความที่บันทึกไว้ตลอดทั้งอุปกรณ์ของคุณหรือไม่? ลงทะเบียน หรือลงชื่อเข้าใช้
Holy Bible, Kiswahili Contemporary Version™ (Neno: Biblia Takatifu™) | Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.
Biblica® Cross Reference System | Copyright © 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.