Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

KutakaMfano

The Quest

SIKU 7 YA 7

Katika maswali manne ya kwanza, Mungu anashikilia taa kwa ajili ya mwenye mwili kujichunguza kusiana na uhusiano wake na Mungu: Uko wapi? Nani alikuambia wewe kuwa? Una tafuta nini? Kwa nini una ogopa? Kinyume chake, ni kwa kiasi gani swali litachukua mshangao wa kutafuta ukweli katika uchunguzi binafsi.



"Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je, Baba yenu wa mbinguni hatazidi sana kuwapa.....?" Luka 11:13a



Krisyo anatoa jibu kupitia msingi wa swali: Si zaidi sana?



Zaidi sana.



Lile swali la maneno matatu na jibu siku zote linatoa mwendelezo wa tumaini.



Mlinganisho kati ya maneno ya Luka na maneno ya Mathayo katika kipande hiki cha mafundisho ya Yesu i wa kufurahisha. Soma Mathayo 7:7-11. Unafanya nini kati ya hayo?



Katika maneno ya kufunga kitabu cha Matendo ya Mitume, Luka alimtaja Roho Mtakatifu zaidi ya mara hamsini na tano. Je, Matendo ya Mitume 10:45 una umuhimu gani maalum?



Baada ya yote aliyoyaona Luka, aliyoyasikia na aliyoyapitia, si ajabu chini ya uvuvio wa Mungu injili yake inasomeka " je, Baba aliye wa mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?" (Luka 11:13). Alijua kwa uhakika kwamba hakuna zawadi duniani kama Roho Mtakatifu. Fikiria daktari ambaye amejenga taaluma kutoka katika mfumo wa kisayansi akisimama na kuona Roho Mtakatifu akishinda maelezo yote ya sheria za asili. Luka hakuwa mjinga. Alikuwa mahiri katika kupima matokeo ili kujua chanzo. Aliona udhihirisho mwingi wa Roho Mtakatifu katika neno, uponyaji, na matendo na ambayo yaliandikwa na Mungu ili kuwa na kumbukumbu ya kudumu ya miujiza iliyoletwa na Roho huyo huyo.



Kumbuka, Mungu ni mtoaji. Katika maneno ya Warumi 8:32, " Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sis sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? Tunaweza kushuhudia kwa zawadi za muda Mungu alizotupa mpaka sauti zetu kukauka, lakini jumla ya yote ni katika ulinganifu wa zawadi kuu ys Roho wa Kristo. Katika zawadi hii moja, maisha yetu yote tunaendelea kufungua zingine: faraja yake, furaha yake,kuchaguliwa kwake, kutiwa nguvu kwake, uongozi wake, upendo wake. Katika haya hakuna mwisho.


siku 6

Kuhusu Mpango huu

The Quest

Katika siku hizi 7 za kusoma na kujifunza, Beth Moore anatumia maswali kutoka katika Maandiko Matakatifu ili kukuongoza kwenye uhusiano wa ndani zaidi na Yeye anayekujua vizuri. Alama za uandishi zilizopotoka mwisho wa s...

More

Tungependa kumshukuru Beth Moore na LifeWay Women kwa kutupa mpango huu. Kwa taarifa zaidi tembelea: http://www.lifeway.com/thequest

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha