Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Yote ni Utulivu: Kupokea Pumziko la Yesu Krismasi hii Mfano

All Is Calm: Receiving Jesus' Rest This Christmas

SIKU 2 YA 5

Siku ya Pili: Kumbuka Wema wa Mungu 



Sote tunaugua usahaulifu wa kiroho, tunasahau Mungu ni nani na yale aliyotutendea kila siku. Kama wewe, hata mimi lazima nijikumbushe kila mwaka Yesu ni nani na mbona kuzaliwa kwake ni miujiza—si kwamba akili yangu haijui bali ni kwa sababu moyo wangu unaacha kushangazwa. Kama msemo wa jadi unavyosema, mazoea huleta dharau, na, mioyo yetu yanaacha kustaajabu. 



Hii ni sehemu ya sababu Wanaisraeli waliambiwa wakumbuke miujiza ya Mungu mara kwa mara: ili wao na watoto wao wasisahau, aidha waendelee kufahamu kwamba Mungu alikuwa karibu nao na ni mwenye nguvu. 



Tunapotarajia msimu wa Krismasi na mipango yote inayohusiana na msimu huu, ni rahisi kusahau na badala yake kujipata kufikiria sherehe pekee. Kwa hivyo ni lazima tuamue kimakusudi kukumbuka wema wa Mungu: Mungu ni nani na yale aliyoyatenda. 



Njia njema ya kufanya hivyo ni kutafakari kuhusu majina yake, msimu wa Krismasi utakuwa mtamu zaidi ukigundua njia ambazo Yesu anazidi kuwa karibu nasi hata wakati huu. 



Kutafakari kuhusu majina ya Yesu ni kama kuzungusha almasi katika jua, unaweza kujua sifa tofauti za hulka yake, kila mmoja ni njema kivu yake, lakini zikiwekwa pamoja zinaleta picha inayopendeza mno ya Mwana wa Mungu aliyekuwa mwanadamu ili kutuokoa. 



Kwa hivyo nakualika usite na ukumbuke wema wa Mungu kwa kutafakari majina ya Yesu, yaliyotajwa katika utabiri mbalimbali unaokaririwa sana kuhusu Mwokozi wetu: 



Yesu ni Immanueli, Mungu aliye nasi, Muumbaji anaye utukufu na nguvu na mamlaka yote ilhali alichagua kuja ulimwengu wetu kama kitoto kichanga ili kuishi na wapendwa wake na kurejesha uhusiano wetu na yeye.



Yesu ni Neno la Mungu, ufunuo na uwasiliano kamili wa Mungu, na ujumbe ulio halisi na wa kibinafsi zaidi kutoka Mungu, na unapatikana na yeyote anayemtafuta.



Yesu ni Mtakatifu wa Mungu, mng'aavu kwa ukuu na mwenye amri kwa mamlaka, asiyekosa, ambaye utukufu wake haututishi bali unatupa sababu ya kutumaini kwani ni yeye pekee anayetupa uadilifu wa kiungu kama vazi na amani.



Mwaliko: Ni jina lipi la Mungu ni tofauti kwako? Sita kidogo na tafakari kuhusu ukwasi wa hulka yake, kisha kariri ama andika njia ambazo Jina lake linakupata penye uliko leo. 


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

All Is Calm: Receiving Jesus' Rest This Christmas

‘Huu ni msimu wa furaha, lakini pia hakuna muda.  Jitenge kwa muda mfupi ya mapumziko na ibada ambao utakulisha unapofanya kazi ya furaha msimu huu. Mpango huu wa siku tano umetoka kitabu Kufungua Majina ya Yesu: Mafunzo...

More

Tungependa kushukuru Moody Publishers kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://onethingalone.com/advent

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha