Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Fedha na matumizi yake kanisani ni jambo nyeti kwa jinsi watu wanavyopokea ujumbe wa kikristo na hivyo kupanuka kwa Injili. Kwa hiyo Paulo alikuwa makini sana alipopanga mkusanyiko wa msaada kwa Wakristo wa Yerusalemu na ni watu gani watakaoutekeleza. Analenga uwazi, ukweli na uwajibikaji katika mambo yote. Haya yaliwezekana kwa vile hawa wote walijitoa kwanza kwa Yesu Kristo. Hivyo waliepuka mianya yote yenye kusababisha wenyewe na wengine kujikwaa. Tafakari maana ya m.20-21 kwako:Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya karama hii tunayoitumikia; tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz
