Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mbazi za YesuMfano

The Parables of Jesus

SIKU 2 YA 36

MJENZI MWENYE BUSARA NA MJENZI MPUMBAVU
Hii ni mbazi ya kwanza ya kweli katika Luka na Mathayo. Yesu anatupa changamoto tuchunguze jinsi ambavyo tunajenga maisha yetu, na kujiuliza msingi ambao tunaujengea maisha yetu.

Tunajenga maisha yetu kimakusudi katika yasiyohamishika, ama tunaruhusu hali zinazotuzunguka na matukio kuwa msingi ambao unahama kila wakati? Je, unajua msingi unaojengea maisha yako, Mungu ama matakwa yako, fikra zako na ndoto zako?

Ni mara ngapi unasoma na/au kusikiliza mafunzo ya Mungu? Ni mchakato upi unatumia ili uyatekeleze katika maisha yako? Unajaribu kujenga maisha yako kwa kazi ya Mungu peke yako ama uko katika kikundi cha "wajenzi?" Kuna sehemu za msingi wako ambazo zinahitaji kubomolewa na kujengwa upya? Usiwache siku nyingine ipite bila kuwa na nia kuhusu jinsi unavyojenga maisha yako kwa Kristo!

Kuhusu Mpango huu

The Parables of Jesus

Mpango huu utakuwezesha kusoma mbazi za Yesu na kuchunguza maana ya mafunzo yake kwako! Unaweza kuendelea na mpango wako ulipoachia kwani imerahisishwa kufika ulipokuwa. Hii itakupa wakati kutafakari na kuhamasishwa na upendo na nguvu wa Yesu!

More

We would like to thank Trinity New Life Church for this plan. For more information, please visit: http://www.trinitynewlife.com/