Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

SIKU 9 YA 31

Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu(m.21).Maana yake ni kwamba Yesu amekuja na mambomapya.Mafarisayo(m.18) ni kundi la kidini. Walijiona kuwa wafuasi halisi wa dini ya Kiyahudi. Walikuwa na mkazo wa kuifuata sheria ya Musa kwa jinsi ilivyofafanuliwa katika mapokeo ya wazee. Hayo mapokeo Yesu aliyakataa, kwa mfano sheria zao za kufunga na kushika sabato(rudia m.18-20 na m.23-28). Kwa Yesu haya yalikuwa ni kama vazi kuukuu. Ila sheria ya Musa aliithibitisha, kwa mfano katika Mt 5:17-20:Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz