Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Yesuakawafundisha(m.13). Ni kweli kwamba alifanya miujiza mingi na kuwaponya wengi. Hata hivyo jambo la kwanza na la msingi kwa Yesu kila wakati lilikuwa ni kuhubiri na kufundisha. Kwa hiyo imeandikwa katika m.2 kwambawakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake(m.2). Zaidi ya yote alitaka watu waponekirohoili wapate uzima wa milele! Siku hiyo Lawi wa Alfayo alipata kupona kiroho. Yesu alipomwita akaitika. Akamfuata na kumpokea kama Mwokozi wake! Fundisho ni hili ambalo Yesu analitia mkazo katika m.17 akisema:Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.Kama wewe ni mwenye dhambi unaitwa na Yesu! Anataka kukuokoa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz