Soma Biblia Kila Siku 01/2025Mfano

Iletaani mfano wa Yesu juu ya ufalme wa Mungu. Kwa mfano huu anazidi kusisitiza namna ya kulisikia neno lake: [Yesu]akawaambia, Mwaonaje? Taa huja ili kuwekwa chini ya pishi, au mvunguni? Si kuwekwa juu ya kiango? Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila makusudi lije likadhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila makusudi lije likatokea wazi. Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa. Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa(m.21-25). Halafu anaonyesha nguvu ya hilo neno:Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi; akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye. Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke. Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika(m.26-29). Kisha anafananisha ufalme wa Mungu na mbegu ya haradali (m.30-32).Haradalini kiungo katika vyakula. Ni mbegu ndogo sana, lakini mti wake huenea sana. Agizo la Yesu la kueneza Injili walipewa watu wachache sana: [Yesu]akaonekana na wale kumi na mmoja ... akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe(Mk 16:14-15). Lakini leo kuna mamilioni ya Wakristo ulimwenguni! Mfano huu unatutia moyo katika utumishi wetu. Basi,tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio(Gal 6:9-10).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 01/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Januari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Marko na Ezra. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: somabiblia.or.tz