Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

SIKU 27 YA 31

Tukimwomba Mungu katika dhiki zetu, tusiwe na haraka kama Mwimba Zaburi aliyesema mara moja, Nimekatiliwa mbali ya Bwana! Maana alijifunza baadaye kwamba Bwana ana fadhili nyingi na kusitiri watu wake dhidi ya wafitini wenye kutega kwa maneno (m.19-20, Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako ulizowawekea wakuchao; ulizowatendea wakukimbiliao mbele ya wanadamu! Utawasitiri na fitina za watu katika sitara ya kuwapo kwako; utawaficha katika hema na mashindano ya ndimi). Kibinadamu, ni rahisi kukata tamaa na kusema Bwana ameniacha. Lakini uzoefu wa Mwimba Zaburi ukupe kuwa hodari na kupiga moyo konde. Katika fadhili zake, Mungu hawatupi wamwendeao. Je, wataka fadhili na stara ya Bwana? Tafakari m.23: Mpendeni Bwana, Ninyi nyote mlio watauwa wake. Bwana huwahifadhi waaminifu, Humlipa atendaye kiburi malipo tele.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz