Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

SIKU 5 YA 30

Hamkumbuki (m.18)? Wanafunzi walikuwa wameona miujiza mikubwa wakati Yesu alipowashibisha maelfu ya watu. Sasa wako chomboni wakiwa na mkate mmoja tu. Wakasumbukia jambo hili, tena wakabishana. Ni kana kwamba wamesahau yote yaliyopita. Ni wazito kuamini uwezo wa Yesu. Na Yesu akawalaumu. Hata sisi Wakristo wa siku hizi ni wepesi kusahau. Bila shaka kila mmoja wetu angeweza kusimulia jinsi Mungu alivyowahi kumsaidia. Na Yesu hajabadilika. Bado ni yeye yule. Tukumbushane! Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote (Zab 103:2).

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu ku...

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha