Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

SIKU 9 YA 30

Yesu anafundisha kuhusu ukuu katika ufalme wa Mungu: Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote (m.35). Ni tofauti sana na ukuu katika ulimwengu huu. Wanafunzi walitumia kipimo cha ukuu katika ulimwengu huu ambacho ni mamlaka ya mtu. Lakini kipimo katika ufalme wa Mungu ni kutumika kwa mtu. Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi (10:45). Huwa huduma kwa watoto haihesabiki kuwa kazi yenye heshima sana. Ila kwa wafuasi wa Yesu hali inatakiwa kuwa tofauti kabisa. Hiyo Yesu anatufundisha katika m.36-37 kwa namna ifuatayo: Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma. Je, unawapenda watoto?

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu ku...

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha