Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

SIKU 8 YA 30

Huyu kijana alikuwa bubu kwa sababu ya pepo mbaya. Lakini wengine ni bubu kwa sababu nyingine; huenda walikuwa na hali hiyo tangu kuzaliwa. Tusianze kumkemea pepo ikiwa hatuna uhakika kama ni pepo. Kama ni ugonjwa wa kawaida tu, basi, tusiwatie watu hofu ya kuwa na pepo mbaya! Yesu alizungumza na huyu bwana kuhusu tatizo la mwanawe (m.21-24, Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu). Hata leo inabidi kufanyike mazungumzo na wagonjwa au wazazi wao kabla ya kutenda lolote. Hali halisi itaeleweka vizuri zaidi baada ya uchunguzi!

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu ku...

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha