Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

SIKU 3 YA 31

Kwa kutumia Neno la Mungu katika kujipima tunatambua dhahiri kwamba hatuna lolote la kujivuna. Usihofu juu ya mafanikio ya watu wengine. Badala yake endelea kujiuliza, Je, ninaonekanaje mbele ya Mungu? Maisha yangu yanalinganaje na Yesu Kristo? Yesu Kristo ndiye ainuliwe, na sisi tushuke (ling. Yohana Mbatizaji alivyojitambulisha mbele ya Yesu: Mimi sistahili kuilegeza gifamu ya viatu vyake; Lk 3:16). Ni yeye Yesu Kristo wa kutuinua. Fungua milango ya kumjulisha Kristo na si wewe mwenyewe. Ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi(Yer 9:24). Paulo anaandika vivyo hivyo: Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana(1 Kor 1:31).

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu....

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha