Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Maombi HatariMfano

Dangerous Prayers

SIKU 5 YA 7

Nivunje



Ni vizuri kuomba kwa ajili ya usalama na baraka, lakini inakuwaje kama unataka zaidi? Inakuwaje kama unatamani nguvu za Roho Mtakatifu, nguvu kutoka mbinguni, imani isiyotikisika, ukaribu wa kweli na Baba yako? 



Badala ya kumwomba Mungu akutunze, akupe zaidi, na kuyalinda maisha yako, unaweza kumwomba Mungu akuvunje.



Ninapofikiria kuomba maombi haya, " Bwana, nivunje," nakumbuka uzoefu ambao Amy na mimi tulikuwa nao katika kundi letu dogo. Katika siku ya moja ya jumatano yenye upepo mkali na baridi mwezi wa Januari, tuliketi katika chumba chenye joto na wanandoa wengine kama saba au nane hivi tukizungumzia maombi haya ya hatari.



Tulikubaliana kwamba wote tulitaka kuomba —na kumaanisha —lakini hatukuweza kukataa kwamba tuliogopa madhara yake. Mwanamke wa kwanza aliyezungumza alimaanisha lakini alikiri jitihada zilizokuwepo. Mama wa watoto wanne, alimfuata Yesu kwa uaminifu tangu alipokuwa shuke ya upili. Alitumika kwenye huduma ya watoto kanisani, alitoa fungu la kumi kwa uaminifu, alisaidia kulea watoto wa wengine, alihudhuria masomo ya Biblia kila juma, na mara nyingi alijitolea kuomba katika makundi mbali mbali.



Lakini alipokabiliwa na uchaguzi wa kumwomba Mungu amvunje, alikataa. " Samahani, lazima niwe muwazi," alisema. " Sitaki kumwomba Mungu anivunje. Ninaogopa kitakachotokea. Mimi ni mama wa watoto wanne. Ninawapenda sana. Kumwomba Mungu anivunje ni jambo la kutisha kwangu. Je, nikiumwa au nikipata msongo wa mawazo au kutengwa na familia?"  



Watu wengi wengine katika kundi lile dogo walitikisa vichwa kukubaliana naye.



Lakini bado swali langu liko pale pale kwetu sote leo: tunapoteza nini tuking'ang'ania kwenye faraja yetu?



Tunakosa nini kwa kujitoa sana kukwepa maumivu na kukosa faraja?



Yesu alisema, “Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.” (Mat. 16:25). Yesu hatualikia kwenye maisha ya faraja na urahisi, lakini ya kujisalimisha na kujitoa. Matamanio yetu makubwa yasiwe mapenzi yetu yafanyike, lakini mapenzi yake yafanyike. Na Yesu anatualika kufa kwa nafsi zetu, ili tuweze kuishi siku baada ya siku kwa ajili yake. Kuacha maisha yetu ya starehe na maombi ya usalama ili kujua inamaanisha nini kuvunjwa kwa ajili ya wengine.



Kwa kuomba kwa usalama, tunaweza kukosa kitu cha thamani zaidi kuliko usalama wetu na faraja. Hatujui kunaweza kuwa na baraka gani upande mwingine Mungu akituvunja.



Luka alisema “Akatwaa mkate [Yesu], akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” (Luk 22:19). Karibu wasomi wengi wa Biblia wanakubaliana na maagizo ya Yesu ya " kufanya hivi" kunatoa njia kwa waamini kukumbuka, kuheshimu na kusherehekea mauti na kufufuka kwake. Lakini wengine wanaamini kwamba "fanyeni hivi" ya Yesu inamaanisha jinsi tunavyotakiwa kuishi. Itakuwaje kama Yesu alikuwa hazungumzii desturi tunayoifanya kanisani? Itakuwaje kama alikuwa anatualika kuvunjwa na kumiminwa kila siku? Itakuwaje kama tungekuwa na ujasiri, na uthubutu, imani ya kuomba, Mungu, nicunje"?



Hatumkumbuki Yesu tuu wakati wa Meza ya Bwana kanisani. Tunamkumbuka kwa jinsi tunavyoishi maisha yetu kila siku. Mwili wa Yesu ulivunjwa, kwa sababu damu yake ilimwagwa kwa ajili yetu, nasi pia yatupasa kuishi kila siku kwa ajili yake, kuvunjika na kumwagwa.



Hili linaweza lisionekane la kupendeza. Nani anataka "kuvunjwa" na " kumwagwa"? Ni kitu cha kuumiza sana, na duni. Lakini ni kutoa uhai wetu kupata furaha ya kweli. Kuliko kufuata mapenzi yetu, tunajisalimisha kwenye mapenzi yake. Badala ya kujaribu kujaza maisha yetu kwa kila tunachohitaji, tunamimina uhai wetu ili kuleta tofauti katika maisha ya watu wengine.



Uvunjifu wa kweli mbele za Mungu si jambo la mara moja; ni uamuzi wa kila siku. Paulo alisema, “ninakufa kila siku.” 1 Kor‬ ‭15:31‬ ‭‬‬Ina maanisha nini? Kila siku, alichagua kusulubisha tamaa zake mwenyewe ili aweze kuishi kikamilifu kwa ajili ya Mungu. Kama una ujasiri kuomba maombi haya, jitayarishe. Jitayarishe kumjua Mungu, na kujulikana naye, kwa njia ambayo hujawahi kuijua.



Unaweza kuwa salama. Lakini nahisi unahitaji zaidi ya hayo. Nachagua kitu tofauti. Nimejawa na imani, nachukua athari kama za mkulima. Sitamtukana Mungu kwa mawazo madogo au kuishimkwa usalama. Kama kuna baraka upande wa pili wa kuvunjika, basi nivunje.


siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Dangerous Prayers

Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church...

More

Tungependa kumshukuru Mchungaji Craig Groeschel na Life.Church kwa kutupa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea https://www.craiggroeschel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha