Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Maombi HatariMfano

Dangerous Prayers

SIKU 1 YA 7

Kwa nini maombi yako yanapaswa kuwa ya Hatari 



Kama walivyo watu wengi, nahangaika kuomba mfululizo na kwa ufanisi kwa miaka mingi. Hata kwa nia njema, mara nyingi navurugwa au hata kuchoka napoomba. Kama mchungaji kijana, rafiki yangu alinisaidia kunishawishi kwamba sasa ni wakati wa kubadirika. Kwa muda mrefu, nilivumilia maombi yasiyokuwa ya imani lakini nilijua Mungu alitaka zaidi kwa ajili yangu, na nilitaka kumjua Yeye kwa undani zaidi.



“Hey, Craig, bado unaamini Mungu anatenda miujiza?”



“Ndiyo,” nilimjibu.



“Vizuri—kwa sababu maombi yako hayana nguvu.”



Nilijaribu kucheka naye, lakini utani wa rafiki yangu uliniingia--kwa sababu alikuwa sahihi.



Nikaachwa sina la kusema, na sikutoa utetezi wowote nilipokuwa nafikiria ukweli wa mtazamo wake. Sikuweza kukataa kwamba alizungumza siri ambayo nilikuwa naijua lakini sikutaka kukiri: maombi yangu yalikuwa hovyo.



Mpango huu ni kwa kila mmoja anayejisikia amekwama kwenye maombi, akiomba kwa kurudia rudia, kujua ataomba nini, na maombi salama.



Tunamtumikia Mungu anayeweza kufanya zaidi ya tuombavyo au kufikiria. Kwa hiyo ni muda wa kuacha mchezo. Hatukuumbwa kwa maisha ya starehe. Tuna nia na nguvu, tukiagizwa kuubadili ulimwengu kwa njia za nguvu! Naamini mpango huu utakutia moyo kupenya kwenye mipaka na kukuvuvia kuomba kwa hatari na kuishi kijasiri.



Kadri nilivyojifunza Biblia zaidi, nilishangaa maombi yaliyosemwa na watu wa Mungu. Si tuu waliombea mambo ambayo yalikuwa ni binafsi-- kupata mtoto kwa mfano, kwa mfano (1 Sam. 1:27)—lakini pia maombi yao yalikuwa kwa matendo, kwa ajili ya mahitaji na chakula (Matayo. 6:11) kuwakwepa maadui zao (Zab 59:1–2). Wakati mwingine yalionekana kama kumnong'oneza Mungu wa upendo. Wakati mwingine walimpigia kelele kwa uchungu na kukata tamaa.



Maombi yao yalikuwa ya kweli. Kukata tamaa. Makali. Ujasiri. Halisi. Na nilikuwa naomba Mungu anilinde na kubariki chakula changu.



Rafiki yangu alikuwa sahihi.



Maombi yangu yalikuwa dhaifu.



Labda unaweza kulinganisha. Si kwamba huamini katika maombi. Unaamini. Lakini unakwama kwenye mazoea. Unaomba juu ya shida zile zile na maombi yale yale. Kwa njia ileile. Wakati uleule. Kama unaomba kweli. Yawezekana unajua kwamba unahitaji kuomba zaidi. Na kwa kumaanisha. Kwa imani zaidi. Unataka kuzungumza na Mungu na kumsikiliza, kushiriki mazungumzo ya ndani zaidi kama unavyoweza na mwenza wako au rafiki yako. Hakika unapenda hivyo lakini huna uhakika jinsi gani. Kwa hiyo maombi yako yanakuwa salama.



Makavu. Hayana ubora. Yanajulikana. Yanachosha. Yamechacha.



Kushtuliwa na rafiki yangu kulinishawishi kwamba ni wakati wa kubadiri maisha yangu ya maombi. Kwa kuwa muda mrefu, nilivumilia uvivu, kutokuwa na imani, na maombi matupu. Nilijua Mungu anataka zaidi kwa ajili kwangu, na nilitaka nimjue zaidi ki undani, pasipokujali kusita kwangu juu ya nini kitatakiwa kwangu.



Tunatafuta kuwasiliana na Mungu katika uhalisia, katika mazingira magumu, na maombi ya ndani, hatufungi katika utandu wa usalama wa kiroho. Badala yake anaingia kwenye utandu wa nini kilichopo kwa ajili yangu na kutukaribisha kumwamini yeye wakati hatujui kifuatacho kutoka kwake. Siku zingine tunajisikia kubarikiwa. Siku zingine tunakumbana na changamoto, upinzani, na mateso. Lakini kila muda wa maombi ya hatari kutajawa na uwepo wake.



Uko tayari kwa zaidi? Umechoka kuomba kwa tahadhari? Uko tayari kuomba kwa kuthubutu, mwenye imani, kumheshimu Mungu, kubadili maisha, maombi ya kubadirisha ulimwengu?



Kama ndiyo, basi mpango huu wa Biblia ni kwa ajili yako.



Lakini tahadhari. Kutakuwa na matuta. Utakapoanza kuomba maombi kama" nichunguze, nivunje, nitume" unaweza kupita kwenye mabonde. Mashambulizi. Majaribu. Maumivu. Magumu. Kukatishwa tamaa. Hata kuvunjika moyo. Lakini pia kutakuwa na furaha ya imani, mshangao wa miujiza, pumziko la kujisalimisha, na furaha ya kumpendeza Mungu.



Ni muda wa kuacha kuomba kistaarabu



Ni wakati wa kuanza kuongea, kuongea kiuhalisia--na kusikiliza kweli--kwa Mungu.



Ni wakati wa maombi ya hatari.


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Dangerous Prayers

Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church...

More

Tungependa kumshukuru Mchungaji Craig Groeschel na Life.Church kwa kutupa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea https://www.craiggroeschel.com/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha