Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Maombi HatariMfano

Dangerous Prayers

SIKU 2 YA 7

Mapenzi yako yafanyike 



Badala ya marefu, yenye kelele, na yakupendeza, maombi yanayomgusa Mungu ni rahisi, ya uhakika, na yanayotoka moyoni. Lakini rahisi si sawa na salama. Na ndiyo maana nalazimika kuandika haya. Kosa kubwa nalofanya nililolifanya katika maisha yangu ya maombi, sababu ambayo maombi yangu yalikuwa dhaifu, ni kwa sababu niliomba kwa usalama. Nilikuwa kwenye eneo la faraja na Mungu. Sikuwa moto na baridi. Maombi yangu yalikuwa vuguvugu. Lakini salama, maombi ya vuguvugu hayatuvuti karibu na Mungu au kutusaidia kuonesha upendo wake kwa ulimwengu huu.



Maombi kwa asili ni hatari. Wazo hili kuhusu maombi lilinishukia nikiwa nasoma habari za Yesu akizungumza na baba yake katika bustani ya Gethsemane muda mfupi tuu kabla hajayatoa maisha yake msalabani. Akijua kilicho mbele yake, Yesu aliuliza kama kuna njia nyingine yeyote. Ndipo Yesu, si mwanafunzi wa kawaida au mtu katika Biblia, lakini Y-E-S-U, mwana wa Mungu, aliomba maombi magumu na ya hatari ya kujikabidhi: "Bado napenda mapenzi yako yatimizwe, si mapenzi yangu"(Luka 22:42).



Yesu kamwe hatutaki sisi kufanya kitu ambacho yeye hawezi kufanya. Anatuita kwenye maisha ya imani, na si maisha ya faraja. Badala ya kuja kwake kwa ajili ya usalama, urahisi, maisha yasiyokuwa na msongo wa mawazo, mwana wa Mungu anatupa changamoto kuhatarisha maisha yetu kwa kuwapenda wengine kuliko wenyewe. Badala ya kufuata shauku zetu za kila siku, anatutaka tuzikatae kwa ajili ya vitu vya milele. Badala ya kuishi kwa kile tunachokitaka, anatuambia tubebe msalaba wetu kila siku na kufuata mfano wake.



Ninamashaka kwa ajili ya watu wengi, maombi ni kama kununua tiketi ya bahati nasibu, nafasi ya kupata maisha hapa duniani yasiyokuwa na shida, maumivu. Kwa wengine maombi ni kama desturi iliyozoeleka, kama kukariri maneno ya wimbo au wimbo wa shule ya awali walioimba utotoni. Lakini bado wengine wanaomba kwa sababu wanajisikia kimya kama hawaombi. 



Lakini hakuna katika maombi haya yanayoonesha maisha ya Yesu aliyokuja kutupa.



Badala yake, alituita tuache kila kitu ili kumfuata.



Yesu hakuwapa changamoto wengine kuacha mapenzi yao nyuma. Yeye pia aliishi maisha ya imani hatari. Aliwagusa wakoma. Alionesha neema kwa makahaba. Na alisimama kwa ujasiri sehemu ya hatari. Kisha akatuambia kwamba tunaweza kufanya alichokifanya-- na kuzidi.



Na ndiyo maana hatuwezi tuu kumwomba Mungu abariki chakula chetu au "uwe nasi leo."



Tunaambiwa katika Biblia kwamba tunaweza " kukikaribia kwa ujasiri kiti cha enzi cha Mungu wa rehema" (Ebr. 4:16a). Hatutakiwi kukikaribia kwa uoga au kuona aibu-- tunaweza kuja mbele zake kwa kujiamini, uhakika, na ujasiri. Tukiomba namna hii, ndipo " tutapokea rehema yake, na tutapata neema ya kutusaidia tunapoihitaji sana" (Ebr. 4:16b).



Maombi yako yana maana.



Jinsi unavyoomba inajalisha.



Unachoomba ni cha maana.



Maombi. Yako. Yanamgusa. Mungu.


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Dangerous Prayers

Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church...

More

Tungependa kumshukuru Mchungaji Craig Groeschel na Life.Church kwa kutupa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea https://www.craiggroeschel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha