Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Kwanza twasikia kwamba Daudi alianza kuwa na urafiki na Yonathani, mwana wa mfalme Sauli (m.1-4). Jambo hili halikuwa ajabu, maana Yonathani alikuwa ameonyesha imani katika Bwana na ushujaa katika vita kama Daudi: Yonathani akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na twende tukawavukie ngomeni hao wasiotahiriwa; yamkini Bwana atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia Bwana asiokoe, kwamba ni kwa wengi au kwamba ni kwa wachache. … Nao watu wa ngomeni wakamjibu Yonathani na mchukua silaha zake, wakasema, Haya! Ninyi, pandeni juu hapa tulipo, na sisi tutawaonyesha jambo. Yonathani akamwambia yule aliyezichukua silaha, Haya! Panda nyuma yangu; kwa kuwa Bwana amewatia mikononi mwa Israeli.Basi Yonathani akapanda kwa mikono na miguu yake, na mchukua silaha nyuma yake; na hao watu wakaanguka mbele ya Yonathani; na huyo mchukua silaha zake akawaua nyuma yake (1 Sam 14:6 na 12-13). Pili twaona Daudi alivyopanda ngazi haraka sana na kupata nafasi kubwa mbele ya mfalme na mbele ya Waisraeli wote: Daudi akatoka kwenda kila mahali alikotumwa na Sauli, akatenda kwa akili; Sauli akamweka juu ya watu wa vita; jambo hili likawa jema machoni pa watu wote, na machoni pa watumishi wa Sauli pia. Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. … Kwa ajili ya hayo Sauli … akamfanya awe akida wake juu ya askari elfu ... Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye Bwana alikuwa pamoja naye(m.5-7 na 13-14). Mafanikio haya yalithibitisha kwamba amechaguliwa na Bwana. Bwana alikuwa amemfungulia njia, na Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja naye(m.12). Pia mafanikio ya Daudi yalimfanya Sauli kumwonea wivu (m.8-11).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021
