Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Sauli alizidi kumchukia Daudi na kutafuta kila njia ili kumwua, ingawa alikuwa ameapa kwa Yonathani akisema: Aishivyo Bwana, yeye hatauawa (m.6). Hali hiyo ilisababishwa na wivu wake pamoja na mapepo mabaya ya Shetani ambayo Mungu aliruhusu yamsumbue Sauli kwa sababu alimwasi (ona maelezo kwa 1 Sam 16:14-23; somo la 8 katika mfululizo huu). Daudi alilindwa na nguvu ya Mungu akiwa Nayothi pamoja na Samweli na manabii. Habari katika m.20 kuhusu wajumbe aliowatuma Sauli ili wamkamate Daudi, kwamba wakatabiri, ina maana kwamba Roho wa Mungu alikuwa juu yao na kuongoza ulimi wao. Ilipotokea kwa Sauli akachanganyikiwa maana ni mwasi: Sauli akaenda Nayothi huko Rama, na Roho wa Mungu akamjilia yeye naye, akaendelea mbele, huku anatabiri, mpaka kufika Nayothi huko Rama.Naye akavua nguo zake, akatabiri mbele ya Samweli, akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha siku ile(m.23-24).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku 07/2020

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021
