Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10

SIKU 17 YA 31

Mfalme Sauli alikuwa anataka sana kumwua Daudi. Huyo alipokuwa amejificha kwa Samweli na kundi la manabii, Sauli alipata habari, akaja ili amkamate (19:22-23).  Daudi akakimbia tena, akatafuta msaada kwa rafiki yake Yonathani, mwana wa Mfalme. Alikuwa amejaa hofu: Iko hatua moja tu kati ya mimi na mauti(m.3). Inawezekana hata wewe umewahi kunusurika. Au sasa hivi unajiona u karibu na mauti, nawe unaogopa. Mpendwa, usihofu, bali umtumaini Bwana Yesu! Ujikabidhi kwake. Ni Mkuu! Akupenda! Soma Zab 91:1-16, maneno yake yatakutia moyo.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz