Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANOMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANO

SIKU 7 YA 7

MFANO WA UFALME WA MBINGUNI 

44a “Ufalme wa Mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena.

44b Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.”

45 “Tena, Ufalme wa Mbinguni unafanana na mfanya biashara aliyekuwa akitafuta lulu safi.

46 Alipoipata lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza vyote alivyokuwa navyo akainunua.”

"47-48 “Tena, Ufalme wa Mbinguni ni kama wavu wa kuvua samaki uliotupwa baharini ukavua samaki wa kila aina.Ulipojaa, wavuvi wakavuta pwani, wakaketi na kukusanya samaki wazuri kuwaweka kwenye vyombo safi, lakini wale samaki wabaya wakawatupa."

49-50 Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia.

"Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki.Nao watawatupa hao waovu katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.”

“Je, mmeyaelewa haya yote?”

Wakamjibu, "Ndiyo"

Akawaambia,

“Basi kila mwalimu wa sheria aliyefundishwa elimu ya Ufalme wa Mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka katika ghala yake mali mpya na mali ya zamani.”

Yesu alipomaliza kutoa mifano hii, akaondoka.

Andiko

siku 6

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANO

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI-AFRIKA kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://gnpi-africa.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha