Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANOMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANO

SIKU 6 YA 7

KUTAWADHA MIGUU YA YESU

36 Basi Farisayo mmoja alimwalika Yesu nyumbani kwake kwa chakula. Hivyo Yesu akaenda nyumbani mwa yule Farisayo na kukaa katika nafasi yake mezani.

37 Naye mwanamke mmoja kwenye ule mji, ambaye alikuwa mwenye dhambi, alipojua kwamba Yesu alikuwa akila chakula nyumbani kwa yule Farisayo, akaleta chupa ya marmar yenye manukato.

38 Yule mwanamke akiwa amesimama nyuma ya miguu ya Yesu akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake,

kisha akaifuta kwa nywele zake akaibusu na kuimiminia manukato.

39 Yule Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake,

“Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua kwamba ni nani anayemgusa na kwamba yeye ni mwanamke wa namna gani na ya kuwa huyu mwanamke ni mwenye dhambi.”

40 Yesu akanena akamwambia, “Simoni, nina jambo la kukuambia.”

Simoni akajibu, “Mwalimu, sema.”

"41 “Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: Mmoja alidaiwa dinari 500 na mwingine dinari hamsini.Wote wawili walipokuwa hawawezi kulipa, aliyafuta madeni yao wote wawili. Sasa ni yupi kati yao atakayempenda yule aliyewasamehe zaidi?”

Simoni akajibu,

“Nadhani ni yule aliyesamehewa deni kubwa zaidi.”

Naye Yesu akamwambia,

“Umehukumu kwa usahihi.”

44-46 Kisha akamgeukia yule mwanamke akamwambia Simoni,

"“Je, unamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawa miguu yangu, lakini huyu ameninawisha miguu kwa machozi yake na kunifuta kwa nywele zake.Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke hajaacha kuibusu miguu yangu tangu nilipoingia.Hukunipaka mafuta kichwani mwangu, lakini yeye ameipaka miguu yangu manukato.

"

47 Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonyesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.”

48-50 Kisha akamwambia yule mwanamke, 

“Dhambi zako simesamehewa.”

Lakini wale waliokuwa wameketi pamoja naye chakulani wakaanza kusemezana wao kwa wao,

“Huyu ni nani ambaye hata anasamehe dhambi?”

Andiko

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANO

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI-AFRIKA kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://gnpi-africa.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha