Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANOMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANO

SIKU 3 YA 7

YESU AFUNDISHA KUHUSU KUFADHAIKA

25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini, au kuhusu miili yenu, mtavaa nini. Je, maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?

26 Waangalieni ndege wa angani, wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko hao ndege?

27 Ni nani miongoni mwenu ambaye kwa kujitaabisha kwake aweza kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha yake au kuongeza dhiraa moja kwenye kimo chake?

"28 “Nanyi kwa nini kujitaabisha kwa ajili ya mavazi? Fikirini maua ya shambani yameavyo. Hayafanyi kazi wala hayafumi.Lakini nawaambia, hata Mfalme Solomoni katika fahari yake yote hakuvikwa kama mojawapo ya hayo maua."

30 Lakini ikiwa Mungu anayavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba?

31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, mkisema, ‘Tutakula nini?’ Au ‘Tutakunywa nini?’ Au ‘Tutavaa nini?’

32 Kwa maana watu wasiomjua Mungu ndio wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji hayo yote.

33 Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake na haya yote mtaongezewa.

34 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TANO

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadi...

More

Tunapenda kushukuru GNPI-AFRIKA kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://gnpi-africa.org/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha