Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!Mfano

Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!

SIKU 7 YA 7

“Kukutanika   na Wakristo”


Kutia   moyo, upendo na nguvu kwa waamini wengine ni moja ya vipaumbele vya muhimu.   Ukweli ni kwamba tunahitajiana mmoja kwa mwingine. Ndivyo Mungu alivyoweka   iwe. Mungu hataki mtu ye yote awe wa “kwenda peke yake.” 


Ukweli ni   kwamba kule kujenga uhusiano na Wakristo wengine ni jambo muhimu katika kukua   kwetu. Mungu mara zote huweka “miadi ya Ki-Mungu” kwa sisi kuhudumu au kutiana moyo kati yetu. 


Kanuni ya   nguvu katika idadi inafanya kazi hata kwa Wakristo, na kuwa na uhusiano wenye   nguvu na waamini wenzako hutusaidia sisi kukua katika mwendo wetu na Mungu! 


Mpango wa   Mungu wa kuanzisha kanisa la mahali ilikuwa ili wewe kuunganishwa na waamini   wengine. Husika na furahia faida za kutoa na kupokea baraka  kutoka kwa ndugu zako wa kike na kiume   katika Kristo!

siku 6

Kuhusu Mpango huu

Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!

Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako...

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha