Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!Mfano

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!

SIKU 1 YA 6

“Je Mungu   Akuruhusu Wewe Kuingia Mbinguni?”

Fikiria   kwa muda kwamba wakati wako hapa duniani umefika mwisho bila kutazamia. Kwa   mshangao, unajikuta umesimama mbele ya Muumba wako. Katika kuchanganyikiwa na   matazamio na kusisimka ukitazamia hatimaye kuyaona makao yako ya milele,   unasimamishwa mara kabla ya kuingia. Mungu anakuuliza swali linalopenya   moyoni, “Kwa nini nikuruhusu wewe kuingia mbinguni?”

Je utajibu   namna gani?

Ashukuriwe   Mungu, siku ile kuu na ya ajabu itakapofika kwa kila mmoja wetu, Mungu   hatatuuliza sisi kufanya mtihani fulani ili kuingia. Hata hivyo, picha hiyo inaonyesha   sura muhimu, inayoleta tafakari ikikusudia kutusaidia sisi kuelewa vizuri   wokovu. 

Baadhi   wanaweza kujibu swali la Mungu kwa kurejea mambo mazuri ambayo walifanya.   Wengine wataelezea uaminifu wao wa mahudhurio kanisani, na wengine wataweka orodha ya mambo mabaya   waliyoyaepuka. Pamoja na kwamba haya ni mambo muhimu ya maisha ya kila   mkristo, hayatuhakikishii wokovu. Kuna jibu moja tu sahihi kwa swali hili:

“Nimemfanya   Yesu Kristo kuwa Bwana wa maisha yangu, na Amenitakasa dhambi zangu zote.”

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!

Maamuzi mengi katika maisha huwa na athari fulani. Hata hivyo, ni uamuzi mmoja tu ndio muhimu zaidi. Kama unatafuta maelekezo rahisi ya kukuwezesha kuelewa kwa undani juu ya uamuzi huu wa ajabu – zawadi ya bure ya wokov...

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha