Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 30 YA 30

Paulo alijisikia kama mfiwa msibani (m.7), wakati hakujua habari ya Wathesalonike. Kwa hiyo faraja ya Paulo ni kubwa, akisikia wanadumu katika imani. Angalia Paulo anavyomtegemea Mungu katika yote: Kama vile mahangaiko ya Paulo yalivyomfanya awaombee wakati hakujua hali yao, sasa habari zao njema zinamfanya amshukuru Mungu kwa ajili yao. Mungu apewe sifa zote! Maana ni neno lake peke yake lililowahifadhi, ingawa pia Paulo alijibidisha kwa ajili yao. Mapungufu ya imani yao (m. 10) yalitokana tu na muda ule mfupi aliokaa nao (majuma 3).

siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha