Zaburi 119:153-160
Zaburi 119:153-160 Biblia Habari Njema (BHN)
Uangalie mateso yangu, uniokoe, kwa maana sikuisahau sheria yako. Unitetee na kunikomboa; unijalie uhai kama ulivyoahidi. Waovu hawataokolewa kamwe, maana hawajali juu ya masharti yako. Huruma yako ni kubwa, ee Mwenyezi-Mungu, unijalie uhai kama ulivyoahidi. Maadui na wadhalimu wangu ni wengi, lakini mimi sikiuki maamuzi yako. Niwaonapo wahaini hao nachukizwa mno, kwa sababu hawazishiki amri zako. Tazama, ee Mungu, ninavyozipenda kanuni zako! Unijalie uhai kadiri ya fadhili zako. Kitovu cha neno lako ni ukweli, maagizo yako yote adili, yadumu milele.
Zaburi 119:153-160 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Uyaangalie mateso yangu, uniokoe, Maana sikuisahau sheria yako. Unitetee na kunikomboa, Unihuishe sawasawa na ahadi yako. Wokovu u mbali na wasio haki, Kwa maana hawajifunzi amri zako. Ee BWANA, rehema zako ni nyingi, Unihuishe sawasawa na hukumu zako. Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi, Lakini mimi sikiuki shuhuda zako. Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako. Uangalie niyapendavyo mausia yako, Ee BWANA, unihuishe sawasawa na fadhili zako. Jumla ya neno lako ni kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.
Zaburi 119:153-160 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Uyaangalie mateso yangu, uniokoe, Maana sikuisahau sheria yako. Unitetee na kunikomboa, Unihuishe sawasawa na ahadi yako. Wokovu u mbali na wasio haki, Kwa maana hawajifunzi amri zako. Ee BWANA, rehema zako ni nyingi, Unihuishe sawasawa na hukumu zako. Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi, Lakini sikujiepusha na shuhuda zako. Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako. Uangalie niyapendavyo mausia yako, Ee BWANA, unihuishe sawasawa na fadhili zako. Jumla ya neno lako ni kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.
Zaburi 119:153-160 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yaangalie mateso yangu, uniokoe, kwa kuwa sijasahau sheria yako. Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako. Wokovu uko mbali na waovu, kwa kuwa hawatafuti maagizo yako. Ee BWANA, huruma zako ni kuu, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako. Adui wanaonitesa ni wengi, lakini mimi sitaziacha sheria zako. Ninawatazama wasioamini kwa chuki, kwa kuwa hawalitii neno lako. Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; Ee BWANA, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako. Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele.