Zaburi 119:145-152
Zaburi 119:145-152 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike; Nitazishika amri zako. Nimekuita Wewe, uniokoe, Nami nitazishika shuhuda zako. Kutangulia mapambazuko naliomba msaada, Naliyangojea maneno yako kwa tumaini. Macho yangu yalitangulia makesha ya usiku, Ili kuitafakari ahadi yako. Uisikie sauti yangu sawasawa na fadhili zako, Ee BWANA, unihuishe sawasawa na hukumu yako. Wanakaribia wanaonifuatia kwa chuki, Wamekwenda mbali na sheria yako. Ee BWANA, Wewe U karibu, Na maagizo yako yote ni kweli. Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako, Ya kuwa umeziweka zikae milele.
Zaburi 119:145-152 Biblia Habari Njema (BHN)
Nakulilia kwa moyo wangu wote; unijibu, ee Mwenyezi-Mungu, nifuate kanuni zako. Nakulilia, unisalimishe; nipate kuyazingatia maamuzi yako. Naamka kabla ya pambazuko na kukuomba msaada; naweka tumaini langu katika maneno yako. Nakaa macho usiku kucha, ili nitafakari juu ya maagizo yako. Kwa fadhili zako, ee Mwenyezi-Mungu, unisikie; unisalimishe kwa uadilifu wako. Wale wanaonidhulumu vibaya wanakaribia, hao wako mbali kabisa na sheria yako. Lakini wewe u karibu nami, ee Mwenyezi-Mungu, na amri zako zote ni za kuaminika. Tangu zamani, nimejifunza maamuzi yako; ambayo umeyaweka hata yadumu milele.
Zaburi 119:145-152 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike; Nitazishika amri zako. Nimekuita Wewe, uniokoe, Nami nitazishika shuhuda zako. Naamka kabla ya mapambazuko na kukuomba msaada, Naweka tumaini langu katika maneno yako. Nakaa macho usiku kucha, Ili kuitafakari ahadi yako. Kwa fadhili zako uisikie sauti yangu, Ee BWANA, uniokoe. Wanakaribia wanaonifuatia kwa chuki, Wamekwenda mbali na sheria yako. Ee BWANA, Wewe U karibu, Na maagizo yako yote ni kweli. Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako, Ya kuwa umeziweka zikae milele.
Zaburi 119:145-152 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, ninakuita kwa moyo wangu wote, nami nitayatii maagizo yako. Ninakuita; niokoe nami nitazishika sheria zako. Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada; nimeweka tumaini langu katika neno lako. Sikufumba macho yangu usiku kucha, ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako. Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako, Ee BWANA, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako. Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami, lakini wako mbali na sheria yako. Ee BWANA, hata hivyo wewe u karibu, na amri zako zote ni za kweli. Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.