Zaburi 119:121-128
Zaburi 119:121-128 Biblia Habari Njema (BHN)
Nimefanya mambo mema na adili; usiniache makuchani mwa maadui zangu. Uahidi kunisaidia mimi mtumishi wako; usikubali wenye kiburi wanidhulumu. Macho yangu yanafifia nikingojea uniokoe, nikingojea utimize uliyoahidi. Unitendee mimi mtumishi wako kadiri ya wema wako, unifundishe masharti yako. Mimi ni mtumishi wako, unipe maarifa, nipate kujua maamuzi yako. Ee Mwenyezi-Mungu, sasa ni wakati wa kufanya kitu, kwa maana watu wanavunja sheria yako. Mimi, nazipenda amri zako, kuliko hata dhahabu safi kabisa. Kwa hiyo, nafuata kanuni zako zote; kila njia potovu naichukia.
Zaburi 119:121-128 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nimefanya hukumu na haki, Usiniache mikononi mwao wanaonionea. Uwe mdhamini wa mtumishi wako, apate mema, Wenye kiburi wasinionee. Macho yangu yanafifia kwa kuungojea wokovu wako, Na kutimizwa kwa ahadi yako ya haki. Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako, Na amri zako unifundishe. Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe, Nipate kuzijua shuhuda zako. Wakati umewadia BWANA atende kazi; Kwa kuwa wameitangua sheria yako. Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi. Maana nayafuata mausia yako yote, kuwa ya adili, Kila njia ya uongo naichukia.
Zaburi 119:121-128 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimefanya hukumu na haki, Usiniache mikononi mwao wanaonionea. Uwe mdhamini wa mtumishi wako, apate mema, Wenye kiburi wasinionee. Macho yangu yamefifia kwa kuutamani wokovu wako, Na ahadi ya haki yako. Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako, Na amri zako unifundishe. Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe, Nipate kuzijua shuhuda zako. Wakati umewadia BWANA atende kazi; Kwa kuwa wameitangua sheria yako. Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi. Maana nayaona mausia yako yote kuwa ya adili, Kila njia ya uongo naichukia.
Zaburi 119:121-128 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nimetenda yaliyo haki na sawa, usiniache mikononi mwa watesi wangu. Mhakikishie mtumishi wako usalama, usiache wenye kiburi wanionee. Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako, na kuitazamia ahadi yako ya kweli. Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako na unifundishe maagizo yako. Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu ili niweze kuelewa sheria zako. Ee BWANA, wakati wako wa kutenda umewadia, kwa kuwa sheria yako inavunjwa. Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, naam, zaidi ya dhahabu safi, na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili, nachukia kila njia potovu.