Methali 20:8-10
Methali 20:8-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Mfalme mwema aketipo kutoa hukumu, huupepeta uovu wote kwa macho yake. Nani athubutuye kusema: “Nimeutakasa moyo wangu; mimi nimetakasika dhambi yangu?” Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu, vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.
Methali 20:8-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu, Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake. Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu? Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA.
Methali 20:8-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu, Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake. Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu? Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA.
Methali 20:8-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mfalme anapoketi kwenye kiti chake cha ufalme kuhukumu, hupepeta ubaya wote kwa macho yake. Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi; mimi ni safi na sina dhambi?” Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, BWANA huchukia vyote viwili.