Methali 16:1-7
Methali 16:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Binadamu hupanga mipango yake, lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi-Mungu. Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa, lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu. Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake; hata waovu kwa ajili ya siku ya maangamizi. Kila mwenye kiburi ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; hakika mtu wa namna hiyo hataacha kuadhibiwa. Kwa utii na uaminifu mtu huondolewa dhambi, kwa kumcha Mwenyezi-Mungu huepuka uovu. Mwenyezi-Mungu akipendezwa na mwenendo wa mtu, huwageuza hata adui zake kuwa marafiki.
Methali 16:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye.
Methali 16:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye.
Methali 16:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na BWANA. Mkabidhi BWANA lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. BWANA hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi. BWANA huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa. Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha BWANA mtu hujiepusha na ubaya. Njia za mtu zinapompendeza BWANA, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.