Mit 16:1-7
Mit 16:1-7 SUV
Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye.