Mithali 16:1-7
Mithali 16:1-7 NENO
Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na BWANA. Mkabidhi BWANA lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. BWANA hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi. BWANA huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa. Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha BWANA mtu hujiepusha na ubaya. Njia za mtu zinapompendeza BWANA, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.