Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 16

16
1 # Mt 10:19 Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;
Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.
2 # 1 Sam 16:7; Dan 5:27 Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;
Bali BWANA huzipima roho za watu.
3Mkabidhi BWANA kazi zako,
Na mawazo yako yatathibitika.
4 # Isa 43:7; Rum 11:36; Ayu 21:30; Rum 9:22 BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake;
Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.
5Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA;
Hakika, hatakosa adhabu.
6 # Dan 4:27; Lk 11:41 Kwa rehema na kweli uovu husafishwa;
Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu.
7 # Kol 1:10 Njia za mtu zikimpendeza BWANA,
Hata adui zake huwapatanisha naye.
8Afadhali mali kidogo pamoja na haki,
Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
9 # Yer 10:23 Moyo wa mtu huifikiri njia yake;
Bali BWANA huziongoza hatua zake.
10Kukata maneno huwa katika midomo ya mfalme;
Kinywa chake hakitakosa katika hukumu.
11 # Law 19:36 Mizani ya haki na vitanga vyake ni vya BWANA;
Mawe yote ya mfukoni ni kazi yake.
12Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo;
Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki.
13Midomo ya haki ni furaha ya wafalme;
Nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa.
14Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti;
Lakini mtu mwenye hekima ataituliza.
15Kuna uhai katika nuru ya uso wa mfalme,
Na fadhili zake ni kama wingu la masika.
16Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu?
Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha.
17 # Mit 4:24-27; Isa 35:8; Mdo 24:16 Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu;
Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.
18Kiburi hutangulia uangamivu;
Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
19Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini,
Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.
20 # Isa 30:18 Atakayelitafakari neno atapata mema;
Na kila amwaminiye BWANA ana heri.
21Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara;
Utamu wa maneno huongeza elimu.
22Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao;
Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
23 # Mt 12:34 Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake;
Huzidisha elimu ya midomo yake.
24Maneno yapendezayo ni kama sega la asali;
Ni tamu nafsini, na afya mifupani.
25 # Mit 14:12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu;
Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
26Nafsi yake mfanya kazi hujifanyia kazi;
Maana kinywa chake humtia bidii.
27Mtu asiyefaa kitu huchimba shimo la madhara;
Katika midomo yake mna moto uteketezao.
28Mtu mshupavu huondokesha fitina;
Na mchongezi huwafarakanisha rafiki.
29Mtu mkali humshawishi mwenzake;
Humwongoza katika njia isiyo njema.
30Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka;
Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya.
31Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu,
Kama kikionekana katika njia ya haki.
32Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa;
Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.
33Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo;
Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 16: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha