Wakolosai 1:1-2
Wakolosai 1:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Timotheo, tunawaandikia nyinyi watu wa Mungu huko Kolosai, ndugu zetu waaminifu katika kuungana na Kristo. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
Shirikisha
Soma Wakolosai 1Wakolosai 1:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu, kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
Shirikisha
Soma Wakolosai 1