Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wakolosai 1

1
Salamu
1 # Efe 1:1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu, 2#Rum 1:7; Efe 1:2 kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
Paulo amshukuru Mungu kwa ajili ya Wakolosai
3 # 1 Kor 13:13; Efe 1:16; 1 The 1:2,3 Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea; 4#Efe 1:15 tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote; 5#1 Pet 1:4; Efe 1:13,18 kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni; ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili; 6#1 Tim 3:16; Efe 1:13 iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda na kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli; 7#Kol 4:12; Flm 1:23 kama mlivyofundishwa na Epafra, mwenzi wetu mpendwa, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu; 8naye alitueleza upendo wenu katika Roho.
9 # Efe 1:8,9,15-17; Flp 1:9 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; 10#Efe 1:17; 2:10; 4:1; Flp 1:27 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; 11#1 Kor 1:5; Efe 1:18,19; 3:16 mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na subira ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha; 12#Efe 1:11,18 mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. 13#Kol 2:15; Lk 22:53; Efe 2:2; 6:12; 1:6 Naye alituokoa kutoka kwa nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa; 14#Efe 1:7 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi.
Ukuu wa Kristo
15 # Ebr 1:3; 2 Kor 4:4; 1 Tim 6:16; Yn 1:18 Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16#Yn 1:3,10; Efe 1:10,21 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au milki, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17#Mit 8:25-27; Efe 1:22 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 18#Efe 1:22-23; 4:15; 5:23; Mdo 4:2; 26:23; Ufu 1:5 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 19#Efe 1:23; Kol 2:9; Yn 1:16 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; 20#Efe 1:7,10; 2:13,16; 1 Yoh 2:2 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni. 21#Efe 2:1,12; 4:18; Rum 5:10 Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmetengwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; 22#Efe 2:11,14,16; 5:27 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; 23#Mk 16:15; 1 Tim 3:16; Efe 3:17; Ebr 3:14 mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa kwa viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nilikuwa mhudumu wake.
Nia ya Paulo kwa Wakolosai
24 # Efe 3:1,13 Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake; 25#Efe 3:2,7,8 ambalo nimefanywa mhudumu wake, kulingana na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu; 26#Rum 16:25,26; Efe 3:3,5,9,10 siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; 27#1 Tim 1:1; Rum 16:25; Efe 3:9; 1:18 ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu 28#Efe 4:13 ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. 29#Flp 4:13; Efe 3:7,20 Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.

Iliyochaguliwa sasa

Wakolosai 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha