1 Samueli 15:34-35
1 Samueli 15:34-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, Samueli akaenda Rama; na mfalme Shauli akarudi nyumbani kwake huko Gibea. Tangu siku hiyo, Samueli hakumwona tena Shauli, mpaka siku alipofariki. Hata hivyo Samueli alimlilia Shauli. Naye Mwenyezi-Mungu alisikitika kwamba alikuwa amemtawaza Shauli mfalme juu ya Israeli.
1 Samueli 15:34-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli. Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye BWANA akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.
1 Samueli 15:34-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli. Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye BWANA akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.
1 Samueli 15:34-35 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha Samweli akaenda Rama, lakini Sauli akapanda nyumbani mwake huko Gibea ya Sauli. Hadi siku Samweli alipofariki hakuenda kumwona Sauli tena, ingawa Samweli alimwomboleza. Naye BWANA alihuzunika kwamba alimfanya Sauli kuwa mfalme juu ya Israeli.